Monday , 23rd Nov , 2015

Kuongezeka kwa dawa bandia za mimea na uanzishwaji holela wa maduka ya viwatilifu katika maeneo ya vijijini kumetajwa kuwa kikwazo kikubwa katika kuendeleza kilimo na kukuza uzalishaji.

Kuongezeka kwa dawa bandia za mimea na uanzishwaji holela wa maduka ya viwatilifu katika maeneo ya vijijini kumetajwa kuwa kikwazo kikubwa katika kuendeleza kilimo na kukuza uzalishaji.

Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya ukaguzi na udhibiti wa viwatilifu TPRI Epifania Kimaro amesema kuwa taasisi hiyo inalojukumu kubwa la kuwasaidia wakulima lakini bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya utekelezaji majukumu yake.

"Wakulima wanapulizia viwatilifu katika mimea kwa kupitiliza kiwangi kinachotakiwa na hivyo kuharibu ubora wa mazao na kutokidhi kiwango cha kimataifa kilichowekwa na WHO" alisema Kimaro.

Kwa upande wao watafiti kutoka TPRI wamesema tatizo kubwa lipo kwa wafanyabiashara wasio waadilifu wanatumia dhana ya biashara huria bila kujali kuwa wanaathiri uchumi wa wakulima pamoja na afya za binadamu.

Wakizungumza katika mkutano uliowakutanisha wadau wa kilimo kujadili changamoto zinazowakabili wakulima ikiwemo wakaguzi wa kilimo kufanya kazi maeneo ya mijini na bila kwenda vijijini wadau hao wamesema wataalamu wa kilimo wanatakiwa kutembelea maeneo yote na kuhakikisha wakulima wanazingatia kilimo cha kiasasa na chenye tija ili kuongeza uzalishaji.