Wednesday , 8th Jul , 2015

Wakizungumza na kituo hiki kwa nyakati tofauti mjini Njombe, wafanyabiashara wamesema kuwa siku hiyo hapo zamani ilikuwa inafanyika kwa maonyesho makubwa na kuchochea maendeleo pampoja na kutangaza bidhaa zinazo zalishwa mikoani

Sehemu ya wafanyabiashara wajasiliamali kutoka nchini Tanzania wakionyesha bidhaa zao kwenye Maonyesho hayo ya Kimataifa.

Akizunguza kwa niaba ya wenzake Tupelile Ngiluka mkazi wa Njombe ametoa ushauri kwa serikali kuona namna ya kuratibu maonesho hayo kufanyika mikoani kwa kuwaunganisha wafanyabiashara ili kujitangaza wao wenyewe pamoja na mkoa kwa ujumla

Ameongeza kuwa ni bora utaratibu wa zamani ukarejea wa kufanywa maonyesho hayo kila mkoa au kuwahamashwa kitaifa ili kila mkoa unufaike na maonyesho hayo.

Katika hatua yingine amesema kuwa jumuiya ya wafanyabiashara mkoa wa njombe ambayo imeanzishwa hivi karibuni inatakiwa kuhusika moja kwa moja katika kuandaa maadhimisho hayo kwa lengo la kuwauunganisha wafanyabiashara kote nchini.

Pamoja na mambo mengine lakini pia Giluka ameitupia lawama serikali kwa kutumia nguvu kubwa kuandaa maonesho ya wakulima nane nane huku ikitelekeza maadhimisho ya sabasaba.