Wednesday , 4th Mar , 2015

Wafanya biashara katika miji ya makambako na njombe Hapo jana wameendesha mgomo wa masaa sita kwaajili ya kuungana na mfanyabiashara mwenzao Mekisoni Sanga ambaye kesi yake ilikuwa ianze kusikilizwa katika mahakama ya wilaya ya njombe

Kibao cha Umoja wa Wafanyabiashara wadogo Mkoani Njombe.

Mekisoni alifikishwa mahakama ya wilaya ya Njombe February 6 kwa kosa la kuwagomea maofisa wa mamlaka ya kukusanya mapato kanda ya mbeya TRA waliofika katika eneo lake la biashara kwa lengo la kumkagua biashara yake

Hata hivyop kesi hiyo imeahirishwa kusikizwa hii leo kutokana na wakili wa TRA Kutofika mahakamani hapo na itasikilizwa tena april 8 mwaka huu kwa upande wa mashahidi

Akizungumza mbele ya wafanya biashara hao baada ya kutoka mahakamani katika ukumbi wa turbo mjini njombe mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara hao mkoa wa njombe TCCIA BW Oraph mhema amewataka wafanyabiashara hao kuendelea kuungana Katika kupigania haki kwa kuwa serikali inaendelea kuwakandamiza

Pia amesema pamoja na kupinga uonevu huo, pia wanapinga mfumo wa ukusanyaji wa kodi kwa ujumla unaotumika kwa sasa hasa kutumia mashine za kielektoniki (EFD) pamoja na TRA kutumia madalali kukusanya kodi, ambao wamekuwa wakisababisha usumbufu kwa wafanyabiashara kwa kufunga maduka yao ovyo kwa makufuli

Kwa upande wa mwenyekiti wa jumhia ya wafanyabiashara tawi la makambako bw sifael sigala amesema kuwa lengo kuanzisha umoja huo ni kutetea unyanyasi wa wafanyabiashara ambao wamekuwa wakilipa kodi sisizo ifikia serikali na kuishia kwa watu fulani

aidha amesema kutokana namaafisa wa mamlaka ya kukusanya mapato (TRA) kuto kuwa na majibu sahihi ya ongezeko la kodi kwa asilimia wameazimia kukutana na kamishna wa biashara taifa ifikapo machi13 mjini makambako ili kupata majibu ya yakinifu Juu ya ongezeko hilo

Katika mkutano huo kumefanyika uchaguzi wa viongozi wa muda wa jumhia ya wafanyabiashara tawi la Njombe ambapo Onesmo Benedicto amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa jumhia hiyo ambaye anasema mifumo ya sheria za ukusanyaji kodi hapa nchini ni kanadamizi kwa wafanyabiashara na kwamba taizo hilo ni la kitaifa

Mgomo mwingine wa wafanyabiashara unataraji kufanyika machi5 ambapo wafanyabiashara watafunga maduka na kuelekea mahakamani kufuatilia mwelekeo wa kesi ya mwenyekiti wa jumhia ya wafanyabiashara taifa John Minja ambayo itasikilizwa mkoani Dodoma