Rais wa Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (CHAUKIDU), Prof. Lioba Moshi.
Mpango huo wa miaka mitano unanuia kuimarisha matumizi mapana ya lugha ya Kiswahili kwa kubuni taasisi na asasi za Kiswahili katika nchi za Jumuiya ili kukuza na kueneza lugha hiyo ya kwanza ya kiafrika inayozungumzwa na watu wengi.
Hata hivo katika eneo hilo kumekuwa na changamoto ya viwango vinavyotofautiana vya Kiswahili.
Mkakati huo kati ya mambo mengi umechagiza kubadilishana kwa wataalamu na mitaala kama sehemu ya kusawazisha viwango hivyo.