Nyumbu wa Masai Mara wanaohamahama kutoka Tanzania kwenda Kenya na kurudi.
Kongamano hilo limeandaliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya Anga za Juu (UNOOSA) kwa ushirikiano na serikali ya Kenya.
Taarifa iliyotolewa na UNOOSA imesema kuwa bayoanuai na viumbe pori vinakabiliwa na hatari kutokana na shinikizo la mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira na uhalifu wa viumbe pori kote duniani.
Kongamano hilo la Nairobi litaangalia jinsi teknolojia ya angani inavyoweza kutumiwa katika kufuatilia, kutathmini na kudhibiti bayoanuai na mazingira, kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za maendeleo endelevu na mazingira endelevu.