
Waandishi wa habari wakiandamana jana nchini Kenya
Takribani waandamanaji 100 walijitokeza mjini Nairobi huku makundi mengine wakiandamana maeneo ya mashariki ya Kitale, Eldoret na Kusini Magharibi Nakuru nchini humo.
Maandamano hayo yamekuja siku moja baada ya mwandishi wa habari wa kujitegemea wa Kitale Dennis Otieno kuuawa kwa kupigwa risasi na wanaume watatu waliokuwa na silaha, katika kile ambacho wafanyakazi wenzake wanasema kinahusishwa na kazi yake.
Wiki iliyopita mwandishi mwingine wa habari wa Standard Media John Masha alizimia na kufariki katika kile familia yake inachosema alilishwa sumu.
