Friday , 13th Mar , 2015

JESHI la Uhamiaji Tanzania, mkoa wa Njombe limetoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za vitendo vya uhamiaji haramu hasa kipindi hiki cha kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura zoezi ambalo linaendelea mkoani humo.

Kamishina msaidizi na kamanda wa Uhamiaji mkoa wa Njombe Rose Mhagama

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe kamishina msaidizi na kamanda wa Uhamiaji mkoa wa Njombe Rose Mhagama, amesema kuwa katika zoezi hili linagusa watanzania na kuwa watu wasiowatanza nia hawatakiwi kujiandikisha.

Amewataka makarani wa uandikishaji wa daftari la kudum u kuwa makini na uchukuaji wa taarifa kwa raia pindi wanapo andikisha kuwabaini watu wasio stahili Licha kueleza kuwa hawajaweza kumbaini mtu yeyote ambaye hana sifa tangu zoezi lilipo zinduliwa Februari 23 mjini makambako

Kuhusu hali ya wahamiaji haramu katika mkoa wa njombe na hyasa mipakani amesema kuwa wameendelea kufanya dolia katika maeneo ya pembezoni na mijini hasa wilaya ludewa ambayo inapakana na nchi ya malawi na mji wa makambako amabao Unapitiwa na barabara kuu ya kuelekea nchi za kusini mwa tanzania.