Friday , 13th Jun , 2014

Vyuo vya Elimu ya Juu nchini vimetakiwa kubuni mitaala itakayowezesha kuwandaa vijana kuwa na utaalamu unaohitajika katika soko la ajira, kuliko ilivyo sasa ambapo wahitimu wengi humaliza vyuo huku wakiwa na vigezo visivyohitajika na waajiri.

Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dkt Shukuru Kawambwa.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam leo na Mkurugenzi wa taasisi ya Mikono Speakers Bw. Deogratius Kilawe ambaye amesema utafiti uliofanywa na taasisi yake umebaini kuwa vyuo vinatoa lundo la maarifa ambayo hayahitajiki na waajiri.

Kilawe ametaja moja ya mfano wa kozi hizo ni ile ya shahada ya kwanza katika fani ya utalii katika mahoteli, kozi aliyosema haitoi mazingira mazuri kwa wahitimu kwani wengi wao huishia kuajiriwa katika nafasi za chini sana ambazo haziendani na ukubwa wa taaluma yao.