
Wanafunzi wa elimu ya juu
Akitoa tamko hilo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa kitengo cha Upangaji na Utoaji wa Mikopo, Dkt Veronika Nyang’ende amesema taratibu za bodi hiyo zinataka vyuo vikuu kuwasilisha matokeo ya wanafunzi haraka iweze kanavyo kabla ya vyuo kufunguliwa.
“Kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo mwaka 2018/2019 kuna nafasi zaidi ya 83 elfu, wanafunzi hawa hupangiwa mikopo baada ya kupatikana kwa matokeo yao ambayo yanatakiwa yafikishwe bodi ya mikopo kwa wakati.” amesema, Dkt Veronika.
Aidha Dkt Veronika amesema, “lazima yawe yamepitia kwa mamlaka husika kwa maana lazima yapite kwa mamlaka husika ikiwemo kuambatana na barua kutoka kwa mkuu wa chuo. Mpaka sasa kuna vyuo karibu 10 havijaleta matokeo kwa maana hiyo wanaweza kupelekea wanafunzi wake kutopata fedha zao.”
Dkt Veronika amesema “matokeo yanatakiwa yaletwe siku 30 kabla ya chuo kufunguliwa ili bodi iweze kumfikishia fedha zake.”