Wednesday , 7th Oct , 2015

Vijana mkoani Iringa wamekumbushwa kufuatilia na kuchambua sera za vyama vya siasa katika kipindi hiki cha kampeni ili kuepukana na vitendo vya rushwa toka kwa wagombea.

Mwanasheria wa TAKUKURU Bi. Restituta Kessy

Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) makao makuu jijini Dar-es Salaam Bi Dorothea Mrema amesema vijana wanaweza kuchagua viongozi bora ikiwa watasikiliza na kuzielewa vema sera za vyama husika.

Aidha, mwanasheria wa TAKUKURU Bi. Restituta Kessy amevikumbusha vyama vya siasa na wagombea kuzingatia sheria za uchaguzi.

Hata hivyo, mmoja wa maafisa hao wa TAKUKURU kutoka makao makuu Bi. Sarah Chodata amewashauri vijana kujitokeza kupiga kura ifikapo Oktoba 25 ili kupata viongozi waadilifu.