
Hayo yamesemwa bungeni Mjini Dodoma baada ya Mbunge wa Busega Dkt. Rhaphaeli Chegeni kuuliza serikali kuhusu wananchi wa Busega wanavyoteseka kupata maji.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa maji na mwagiliaji Isack Kamwele amesema kwamba katika mwaka wa fedha 2016 & 2017 mradi mkubwa wa maji utajengwa kutoka ziwa viktoria ambapo bomba litakalopita litasaidia vijiji 223 na mradi huo utakamilika baada ya miaka miwili.
Aidha wananchi wanaozunguka bomba gilo kuu kutoka umbali wa kilomita 12 kushoto na kulia nao watapatiwa maji na watu zaidi ya laki 8 wanatarajiwa kunufaika na maji hayo.