Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe
Vijana zaidi ya 2100 waliohitimu mafunzo ya awali ya kijeshi operesheni ya miaka 50 ya muungano nchini, wameagizwa kuacha kujiingiza katika vitendo viovu katika jamii na badala yake wametakiwa kuwa mabalozi wazuri watakaosaidia kuelimisha jamii umuhimu wa kujiunga na jeshi la kujenga taifa nchini (JKT).
Agizo hilo limetolewa na viongozi wa JKT nchini wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi operesheni miaka 50 ya muungano katika kikosi cha 865 KJ cha mgambo JKT wilayani Handeni ambapo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali mkoa wa Tanga pamoja na baadhi ya wazazi.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika shughuli hiyo, ambaye alikuwa mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Tanga Bwana Mrisho Gambo amesema kulingana utaratibu uliowekwa na serikali wa kurejesha wanafunzi wa kidato cha sita kwenda jeshini kabla ya vyuo vikuu, wengine waliojiunga na mafunzo hayo kwa kujitolea watawawekea utaratibu kwa wilaya ya Korogwe kuwatafutia mashamba makubwa ili wajiunge na vikundi vya kilimo kwa lengo la kunufaika na mikopo.