Tuesday , 21st Apr , 2015

Vijana nchini wametakiwa kujitokeza na kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao na kuachana na kutumiwa na wanasiasa kwa manufaa yao binafsi.

mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM (NEC), Anthony Mavunde.

Wito huo umetolewa leo na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM (NEC), Anthony Mavunde kwenye uzinduzi wa tawi la wakereketwa wa Jakaya Kikwete lililopo Mtaa wa Ilazo kata ya Ipagala katika manispaa ya Dodoma.

Aidha amewataka vijana hao kutowachagua viongozi kutokana na fedha zao bali wawachague kutokana na dhamira yao ya ndani ya kuwaongoza.

Kwa upande wake kamanda wa vijana wa tawi hilo, Gombo Dotto amewaomba vijana hao kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwani bila ushirikiano hawataweza kufanikiwa katika kufikia mafanikio

Katika uzinduzi huo Mavunde ametoa mchango wa sh. 500,000 kama mtaji kwa vijana hao ambao wanajishughulisha na shughuli za mama lishe ambapo pia amegawa jumla ya kadi 50 kwa wanachama wapya wa CCM.