Mkurugenzi wa Utafiti wa Utawala bora na huduma za kijamii toka Repoa Dr. Lucas Katera.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Utafiti wa Utawala bora na huduma za kijamii toka Repoa Dr. Lucas Katera na kuongeza kuwa tafiti zinaonesha kuwa madaktari wengi vijijini hawawapi wagonjwa haki ya kuwasikiliza huku wengi uwezo wao ukiwa ni mdogo kwa kukosa mafunzo ya mara kwa mara ya kuwaongezea na kuwajengea uwezo.
Kwa upande wa sekta ya elimu Dkt. Katera amesema kuwa walimu wengi hawana morali ya kufundisha hata katika maeneo ambayo kuna vitabu vya kutosha, mazingira mazuri ya kufundisha.
Hata hivyo Dkt. Katera ameishauri serikali kuwa karibu na watumishi wake hasa walimu na madaktari pamoja na kuwapa motisha na mafunzo ya mara kwa mara ya kuwajengea uwezo na kuamsha morali za utendaji kazi.