Mjumbe wa halmashari kuu ya Taifa ya CCM,na mbunge wa mtama mkoani lini,ambaye pia ni Waziri wa mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh, Bernad Membe
Mjumbe wa halmashari kuu ya Taifa ya CCM,na mbunge wa mtama mkoani lini,ambaye pia ni Waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa,Mh, Bernad Membe anajitokeza mbela ya vyombo vya habari,nakupinga vikali utafiti huo kwa kile alichodai ni kukosa vigezo.
Aidha Mh, Bernard Membe anasema kuwa,utafiti huo haukuzingatia vigezo vya 531 na kuwa utafiti huo umekuja mapema,wakati ambapo hakuna chama kilichomtangaza mgombea wake,huku akidai kuwa utafiti huo umeleta changamoto nchini,huku akipinga kitendo cha kuchanganya wanachama hao toka vyama vyaCUF na CHADEMA vyama anavyovieleza kuanza kupoteza mwelekeo wa siasa ya ushindani.
Utafiti huo wa Twaweza uliotoka hivi karibuni umeonyesha kuwa Mh. Edward Lowassa Mbunge wa Monduli akiongiza kinyang'anyiro hicho huku akifatiwa na Mh. Pinda kwa Upande wa Chama cha Mapinduzi na Dkt. Wilbroad Slaa kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo.