Monday , 7th Jul , 2014

Kukithiri kwa vitendo vinavyosababisha uvunjifu wa amani na matatizo mbalimbali nchini Tanzania kumetajwa kuwa husababishwa na wananchi wenyewe na hupelekea kuathiri kwa kiasi kikubwa ustawi wa taifa na mustakabali wa nchi na vizazi vijavyo.

Wananchi wakiandamana mkoani Mtwara Kupinga ujenzi wa Bomba la gesi

Kukithiri kwa vitendo vinavyosababisha uvunjifu wa amani na matatizo mbalimbali nchini Tanzania kumetajwa kuwa husababishwa na wananchi wenyewe na hupelekea kuathiri kwa kiasi kikubwa ustawi wa taifa na mustakabali wa nchi na vizazi vijavyo.

Akizungumza na EastAfrica Radio Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Mabalozi wa Kimataifa wa Uhisani (RAI) Bw. Felix Switbert ametaja miongoni mwa vitendo hivyo ni pamoja na kukithiri kwa matumizi ya dawa za kulevya, ufisadi, rushwa, migogoro ya ardhi na kutokuwajibika katika kazi.

Hata hivyo Switbert amesema umefika wakati wa kukaa pamoja na kutafuta suluhisho la matatizo badala ya kulalamikia serikali hivyo taasisi hiyo wameandaa kongamano la kitaifa litakalofanyika jijini Dar es Salaam Julai 25.