Tuesday , 29th Dec , 2015

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF limeshirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma katika kampeni ya kuelimisha kuhusu kipindupindu.

Muwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid

Lengo la kampeni hiyo inayotangazwa kupitia mitandao ya kijamii na ujumbe wa simu za mkononi ni kuelimisha jamii kuhusu njia za kujikinga na kipindupindu.

Mojawapo ni kuzingatia usafi wa chakula, kwa kukisafisha na maji salama, kukila mara tu baada ya kupikwa wakati kikiwa bado cha moto na kuhakikisha kiporo kinapashwa moto kabla ya kuliwa.

Njia nyingine ni kunywa maji safi na salama yaliyochemshwa au kusafishwa na vidonge vya klorine kama unavyoeleza ujumbe wa mwanaharakati huyu .

Kwa mujibu wa kampeni hiyo, mtu yeyote anayetaka kuelewa zaidi kuhusu hayo anaweza kutuma ujumbe wa simu ya mkononi, akiandika KIPINDUPINDU kwenda kwa namba 15774 nchini Tanzania.