Tuesday , 10th May , 2016

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), limeeleza wasiwasi wake mkubwa, kuhusu uamuzi ulioripotiwa kutolewa na serikali ya Kenya Ijumaa wiki iliyopita, wa kufunga kambi za wakimbizi nchini humo.

Moja kati ya kambi za wakimbizi zinazopatikana nchini Kenya.

UNHCR imeisihi serikali ya Kenya kufikiria upya uamuzi wake na kujizuia kuchukua hatua yoyote itakayoenda kinyume na wajibu wake wa Kimataifa wa kuwapa hifadhi watu wanaokimbia hatari na mateso.

Kwa mujibu wa taarifa ya UNHCR, imeripotiwa kuwa madhara ya kiuchumi, kiusalama na kimazingira yamesababisha uamuzi huo wa Kenya.

Ikitambua mzigo mkubwa unaobebwa na Kenya, UNHCR imeipongeza pia nchi hiyo kwa kuchangia pakubwa katika kuwapa hifadhi mamia ya maelfu ya wakimbizi wa Sudan Kusini na Somalia kwa kipindi cha miaka 25 iliyopita.

UNHCR imesisitiza kwamba, iwapo uamuzi huo utatekelezwa, wakimbizi wapatao 600,000 wataathirika.

Tags: