Thursday , 23rd Oct , 2014

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO linahaha kunusuru na kurejesha hadhi ya mji mkongwe wa Zanzibar ambao umeingia katika orodha hatarishi ya kutoweka katika urithi wa dunia.

Moja kati ya Majengo yanayopatika Mji Mkongwe Visiwani Zanzibar ambavyo ni Vivutio vya Utalii.

Afisa wa UNESCO Tanzania Moshi Kiminzi amesema shirika hilo kwa kushirikiana na serikali ya Zanzibar na mamlaka ya mji mkongwe wanahakikisha hatua muhimu zinachukuliwa kunusuru mji huo ambao amesema kutoweka kwake kutafuta historia ya eneo hilo muhimu Afrika Mashariki.

Pia Kiminzi amefafanua kile kinachofanywa na UNESCO kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa kutunza mji huo ili usiondoke katika orodha ya urithi wa dunia.

Mji huo ambao ndio kivutio kikubwa cha watalii Zanzibar na ndio chanzo kikubwa cha pato la taifa na visiwan humo ambalo linakuza uchumi kwa kiasi kikubwa.