Thursday , 5th Feb , 2015

Serikali imekiri kuwa  ukosefu  wa  elimu  ni  moja  ya  changamoto kwa  wananchi  na  wafanyabiashara  nchini, hatua  ambayo  imewafanya  washindwe  kutambua  fursa zinapatikana  katika  nchi  za Afrika Mashariki.

Kituo cha kutolea huduma maalum kwa pamoja kilichojengwa Sirari mpakani mwa Tanzania na Kenya

Wizara  ya  ushirikiano wa   Afrika  Mashariki  imekiri  kuwa  ukosefu  wa  elimu  ni  moja  ya  changamoto  kubwa  kwa  wananchi  na  wafanyabiashara  nchini hatua  ambayo  imewafanya  washindwe  kutambua  fursa  zinapatikana  katika  nchi  wanachama  za jumuiya hiyo  ya  Afrika  Mashariki.
 
Naibu  katibu  mkuu  wa  Wizara  ya  Ushirikiano  wa  Afrika  Mashariki Amantius Msole, amesema ukosefu   wa  elimu  miongoni  mwa   watanzania  ni moja  sababu  ambazo   zimesababisha  wafanyabiashara  wengi  kuingiza bidhaa  kwa  njia   za  magendo zikiwemo   zile   ambazo  hazistahili  kulipiwa  kodi  na ushuru mbalimbali.

Msole ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi   na  wafanyabiashara   katika  mpaka   wa  Tanzania  na Kenya  eneo la  Sirari  muda mfupi   baada   ya  kutembelea  vituo  maalum   ya  kutolea  huduma   za   pamoja,
 
Nao   baadhi    ya   wananchi   wakiwemo   viongozi   wa  chama  cha  wafanyabiashara  wenye   viwanda   na  kilimo   TCCIA,
wamesema  ukosefu   wa   elimu   kuhusu   fursa   zilizopo  katika   soko   la  pamoja   la   Afrika  Mashariki  kumewafanya   watanzania  kuwa  watumwa  katika   nchi  wanachama    wa   jumuiya  hiyo.
 
Tayari   ujenzi  wa  vituo   vya  kutolea  huduma  za  pamoja   za   forodha, uhamiaji, polisi  na  idara  nyingine  za  udhibiti  mipakani  umekamilika katika  eneo la  Sirari  nchini  Tanzania  na Isibania  nchini  kenya  lengo  likiwa  ni  kupunguza kero  kwa  pande  hizo  mbili.