Monday , 4th Jul , 2016

Kukithiri kwa watoto wanaozaliwa na mtindio wa ubongo na kuharibika mimba kwa kina mama ni miongoni mwa athari zinazoweza kuikumba mikoa ya Lindi na Mtwara kutokana na kukosa matumizi ya chumvi yenye madini joto.

Chumvi

Hayo yameelezwa na Katibu wa Afya wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mtwara, Ligula, Jenifer Mapembe, baada ya ufunguzi wa semina ya siku moja ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa mkoa huo juu ya athari zitokanazo na matumizi ya chumvu isiyo na madini joto na namna ya kuielimisha jamii.

Aidha, baadhi ya waandishi wa habari waliopata semina hiyo, wametoa mapendekezo yao juu ya mikakati inayopaswa kufanywa na wadau wa afya kwa kushirikiana na wizara pamoja na vyombo vya habari ili kuiokoa jamii kuondokana na matumizi ya chumvi hiyo.

Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamiii, Jinsia, Wazee na Watoto, Omary Gwao, amesema mikakati ya wizara ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wanahabari ili waweze kujua ukubwa wa tatizo na kupanga mikakati ya kuweza kuisaidia jamii.

Sauti ya Katibu wa afya wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mtwara, Ligula, Jenifer Mapembe.