Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha taifa cha Ulinzi ambaye pia ni Mhadhiri wa masomo ya mpango mkakati na historia katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Prof.Eginald Mihanjo
Mkurugenzi wa mafunzo wa chuo cha taifa cha ulinzi ambaye pia ni mhadhiri wa masomo ya mpango mkakati na historia katika chuo kikuu cha Dar es salaam, Prof.Eginald Mihanjo,amesema hayo wakati akizungumza na wanajumuiya wa shule ya sekondari kizuka,ambapo mbali na kuwahimiza watanzania kuona shahada ya kwanza ni sawa na elimu ya msingi ili kumudu ushindani kimataifa.
Ameongeza kuwa tatizo la ukosefu wa nidhamu amelibaini hata kwa wanafunzi anaowafundisha ambao miongoni mwao ni wale wanaoandaliwa kuwa viongozi,na kuhimiza katika kukabiliana na hali hiyo,ni vyema wazazi na walezi wakawalea watoto katika maadili mema tangu nyumbani ili iwe rahisi shuleni na katika maeneo mengine.
K wa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari kizuka inayomilikiwa na jeshi la wananchi wà Tanzania, Kamandi ya Anga, Lut.Kan.George Mwashiga,mbali na kushukuru jeshi hilo kuwapa fursa walimu wake hasa wanajeshi kujiendeleza.
Amesema mbali na kujikita kukuza vipaji vya michezo, katika kuhakikisha agizo la mkuu wao la kuifanya shule hiyo inawaandaa vijana kuwa wazalendo na marubani wa baadaye wa jeshi hilo na mafuñdi wa ndege,wamejipanga mwakañi kujenga maabara tatu za kisayansi zitakazokidhi mahitaji ya elimu ya kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita