Thursday , 8th Dec , 2016

Ukatili wa kijinsia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam umepungua baada ya chuo hicho kupitia kituo chake cha jinsia kutunga sera inayosimamia masuala ya jinsia ambayo imekuwa mwongozo wa kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia chuoni hapo

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

 

Mkurugenzi wa kituo hicho kinachojulikana kama University of Dar es Salaam Gender Centre Dkt. Euginia Kafanabo, amesema hayo wakati wa kongamano la jinsia, lililoandaliwa mahsusi kwa ajili ya kuadhimisha siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia.

Je hali ya ukatili wa kijinsia chuoni hapo ipoje kwa sasa? Naibu Waziri wa Jinsia na Mahitaji Maalumu wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo Pauline Sylvester, amesema idadi ya matukio ya ukatili tangu serikali hiyo iingie madarakani imepungua ikilinganishwa na ilivyokuwa kabla