
Theresa may (Kushoto) akiwa na Narendra Modi
Bi. Theresa ambaye yuko nchini India kwa ajili ya mazungumzo ya kibiashara baada ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya, EU, amesema, tayari nchi yake imefanikiwa kuzivutia nchi nyingi nzuri kwa ajili ya biashara nje ya EU.
Amesema, mpaka sasa maombi tisa kati ya kumi ya visa kutoka India yanakubaliwa, lakini akaonya kwamba raia wa India watakaozidisha muda wa visa watarejeshwa nyumbani haraka.
Serikali ya Uingereza pia ina mpango wa kuwawezesha wafanyabiashara matajiri wa India kuingia nchini humo kwa urahisi