Ugonjwa umepiga hodi jana jioni kwa mgonjwa mmoja mkazi wa kata ya Lamadi kuzidiwa na kupelekwa katika hospital ya mkula iliyo chini ya kanisa na hivyo kuweza kufungulia njia kwa wengine kwa sasa wagonjwa wanazidi kuongezeka na huku kukiwa hakuna eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya wagonjwa hao.
Hali inavyoonyesha uenda ugonjwa huo ukaitesa zaidi wilaya hiyo na hii ni kutokana na wakazi wengi wa maeneo hao kutokuwa na vyoo hasa kando mwa Ziwa Victoria maeneo kama Buyolwa ndogo ambako wakazi walio wengi wanajisaidia katika msitu ulio umbali wa mita chache na ziwa ambalo ndio kiungo kikubwa katika eneo hilo kwani maji utumika kwa shughuli zote za viumbe hai zinazohitajika kutumika.
Akitoa taarifa za uwepo wa ugonjwa huo Mganga Mkuu wa wilaya Hiyo Bw. Godfrey Mbagali alisema kuwa ni kweli ugonjwa huu umetufikia Busega lakini tumesha fanya mikakati kabambe ya kuhakikisha ugonjwa huu ausambai kwa wananchi ili kuweza kuokoa maisha ya wananchi wote.