Sunday , 19th Jun , 2016

Watu saba wamefaiki Dunia na wengine 21 wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kondoa na ya Rufaa ya Dodoma baada ya kuibuka ugonjwa unaohusishwa na ulaji wa vyakula vyenye sumukuvu.

Waziri Ummy Mwalimu akiwasikiliza wananchi katika moja ya Ziara zake

Watu saba wamefaiki Dunia na wengine 21 wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kondoa na ya Rufaa ya Dodoma baada ya kuibuka ugonjwa unaohusishwa na ulaji wa vyakula vyenye sumukuvu.

Akizungumza leo mjini Dodoma,Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amesema ugonjwa huo umeanzia katika wilaya ya chemba baada ya kuikumba familia moja katika kijiji cha Mwaikisabe kata ya kimaha Wilayani Chemba baada ya kula nyama ya ng’ombe aliyechinjwa kwa kluvunjika mguu katika kijiji hicho.

Baadae wagonjwa wengine walianza kupatikanakatika vijiji vya karibu vikiwemo vya Soya,Itolwa,Kelema Balai,Gubali,Chemka,Kintima,Ilesi, na Ubembeni pamoja na Wilaya ya Kondoa huku mbali na watu hao ni pamoja na Mbwa wakubwa watatu,Mbwa wadogo watatu na Paka 1 katika familia hiyo ulipoanzia ugonjwa huo ambao haujatambulika.

Mhe.Ummy Mwalimu amesema ugonjwa huo umekuwa na dalili Kutapika,Kuharisha,Kupata rangi ya manjano machoni na sehemu nyingine za mwili pamoja na kuwa na maumivu ya tumbo na hatimaye kuvimba tumbo kwa kujaa majindani ya muda mfupi.

Waziri Ummy ameongeza kuwa ugonjwa huo hauhusiani na ugonjwa wa Kimeta na Tayari kwa kushirikiana na mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ,wamechukua hatua za kuwatengea wodi maalum wagonjwa hao,kuunda kamati za madawa ,matibabu,maabara,kupeleka wataalam wa afya wilayani Kondoa ,kuchukua sampuli mbalimbali kwa ajili ya uchunguzi ikiwa ni pamoja na nafaka kutoka katika familia hizo.

Aidha,Waziri Ummy Mwalimu amesema Serikali kwa Kushirikiana na Shirika la Afya Duniani WHO,na kituo cha kudhibiti Magonjwa CDC na Ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali kuhakikisha ugonjwa huo haraka ili usiendelee kuwadhuru wananchi wengi Zaidi