Mkuu wa Shule ya Sekondari Bungoni iliyopo Kisarawe Mkoani Pwani, Ally Kwayu.
Hayo yameelezwa na wadau wa elimu wilayani Kilosa mkoani Morogoro , ambapo mkuu wa shule ya sekondari Bungoni iliyopo Kisarawe Mkoani Pwani, Ally Kwayu ametoa wito kwa serikali kutoa motisha kwa walimu wa masomo ya sayansi ili kuwezesha kupata walimu wa kutosha,sambamba na kusimamia kwa ufasaha maabara zinazoendelea kujengwa kwa nguvu za wananchi.
Naye kaimu mkuu wa shule ya sekondari Dakawa, Ipyana Kisalile akibainisha ukosefu wa majengo ya maktaba na changamoto nyingine zimeathiri masuala ya utoaji wa taaluma shuleni
Wadau hao wametoa wito kwa jamii kujenga tabia ya kuzisaidia shule walizosoma zamani ili kuhakikisha changamoto mbalimbali zinatatuliwa na kukuza kiwango cha taaluma kinachotolewa, badala ya kusubiri wazazi na serikali,
Wadau hao wamewataka watu waliosoma katika shule mbalimbali kusaidia shule hizo kitaaluma ambapo wao kama wanafunzi wa zamani wa Dakawa Sekondari, wamejichanga na kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kusaidia kukuza taaluma, ikiwemo projecta, kompyuta ya mpakato yaani laptop pamoja na magodoro.