Friday , 2nd Oct , 2015

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imesema imejipanga vyema kuhakikisha wanawake wote wenye sifa za kupiga kura wanatimiza haki yao ya msingi pasipo bugudha yoyote.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva

Akizungumza na Makundi mbali mbali ya Wanawake leo jijini Dar es salam Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva amesema wameandaa utaratibu mzuri ambao wanawake wajawazito na wanaonyonyesha watapewa kipaumbele siku ya kupiga kura.

Jaji Lubuva ameongeza kuwa tume imetoa maelekezo kwa makarani waongozaji vituoni kutoa kipaumbele kwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha ili wasikae katika foleni kwa muda mrefu.

Hata hivyo jaji Lubuva amewataka wagombea kutumia lugha za staha na kuepuka matusi na kejeli.

Kwa upande wa wanawake wanaoshirika mkutano huo wameitaka tume kuwachukulia hatua wagombea wote wanaotoa lugha za matusi ambapo hata watoto husikia matusi hayo na lugha mbaya za kejeli, Hata hivyo jaji Lubuva amesema ni makosa kimadili kutoa lugha chafu.