MWENYEKITI wa CHADEMA Kitaifa, Mh. Freeman Mbowe (wa pili kulia) akiwatambulisha Mgombea wa Urais wa Umoja wa vyama vinne vya upinzani (UKAWA
Akizungumza jana Mara ya Kutangazwa kuwa mgombea rasmi wa Umoja huo pamoja na Mgombea mwenza kutoka CUF aliechukua kado ya CHADEMA ili kutimiza makubaliano ya Umoja huo Lowassa amesema atatembea nchi nzima na kuhakikisha hakutakua na fujo zozote.
Aidha Mh. Lowassa amewashukuru wanachadema kwa imani waliyomuonyesha ya kuweza kumpa nafasi ya kuipeperusha bendera ya chama hicho pamoja na UKAWA na kuahidi kulipa fadhila hizo kwa vitendo pindi atakapochukua Madaraka
-------NEWS CLIP 10AM SWA TZ 1----------
Kwa Upande wake Mgombea Mwenza wa Mh. Edward Lowassa, Juma Haji Duni amesema ameamua kufanya maamuzi magumu ya kujiunga na chama hicho ili kuitoa CCM madarakani huku akiahidi kudumisha Muungano.
Na Mgombea Pekee wa Urais kupitia Umoja huo kwa Upande wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema uamuzi uliofanyika ni wa busara na unapaswa kuungwa mkono na kusema kuwa bado Mwenyekiti wa chama hicho yupo pamoja nao na hajatangaza msimamo wowote wa kujivua Uenyekiti.