Friday , 29th Jan , 2016

Waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji Charles Mwijage amesema serikali imepanga kujenga uchumi wa nchi kwa upande wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya uchumi wa watu.

Waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji Charles Mwijage

Mhe. ameyasema hayo mkutano wa pili kikao cha tatu Bungeni Mjini Dodoma alipokua akijibu hoja mbalimbali za wabunge walizochangia na kujadili hotuba ya Rais John Magufuli aliyoitoa siku ya ufunguzi wa Bunge la kumi na moja tarehe 20 Novemba 2015 .

Amesema kila mtanzania anajukumu la kusimamia uchumi wa nchi kwani serikali tayari imeanza kusisimamia mazingira bora ya uwekezaji yanapatikana kwa wafanyabiashara.

Aidha Waziri huyo wa Viwanda amesema kuwa Serikali itahakikisha a ajira zinaongezeka nchini kupitia viwanda hasa kwa vijana wanaohangaika kutafuta ajira kila siku.