Wednesday , 1st Apr , 2015

Tume ya haki za Binadamu na utawala bora imepokea kwa masikitiko taarifa ya kuuawa kwa askari polisi wawili waliokuwa kazini na kuibiwa silaha tukio lilitokea usiku wa March 30 huko, Kongowe, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Mwenyekiti wa Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Bahame Tom Mukiria Nyanduga.

Kutokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 14 kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake kwa mujibu wa sheria hivyo kuuawa kwa askari polisi ambao ni walinzi wa usalama na amani wakiwa kwenye majukumu yao ni kitendo cha kulaaniwa na kila mwananchi.

Pia tume imesema imesikitishwana tukio la hivi karibuni la kuvamiwa na kupigwa kwa wafuasi takribani 25 wa chama cha wananchi CUF waliokuwa wakitoka mkutanoni Makunduchi wilaya ya kusini Unguja March 29.

Tume imewataka wananchi kuheshimu haki za binadamu na kuwa na uvumilivu wa kisiasa hususani kipindi hiki ambacho nchi inakabiliwa na matukio m akubwa ya kupigia kura ya maoni Katiba Inayopendekezwa na uchaguzi mkuu.

Aidha tume hiyo imewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi katika kuhakikisha watu waliofanya matukio hayo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo husika ili sheria ichukue mkondo wake.