Thursday , 17th Mar , 2016

Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wameitaka Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoa taarifa ya taratibu zililizofuatwa na Aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Kuwasimamisha kazi wataalamu wa Afya.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akizungumza na wanahabari hawapo pichani,

Hayo yamesemwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii ambao walihoji uhalali wa Wakuu wa Mikoa kuingilia kazi za kitaalamu ambazo kama hautakua makini katika utoaji wa Adhabu unaweza kusababisha matatizo makubwa ndani ya jamii husika.

Kamati hiyo imesema kuwa kitendo kilichofanywa na mkuu huyo wa Mkoa aliyehamishiwa Mkoani Mara Magesa Mulongo ambae aliwasimamisha kazi watumishi katika hospitali ya Butimba wilayani Nyamagana kwa tuhuma za na kusababisha vifo vya makusudi hali iliyosababisha watumishi wengine kugoma kufanya kazi za kuhudumia jamii ikiwa ni pamoja na wao kudai kuwa hawakutendewa haki kwa kusikilizwa juu ya tukio hilo.

Kwa apande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala ambaye alifika kwenye kikao hicho kwa nia ya kutoa taarifa ya wizara ya mwaka 2015/2016 amesema tayari ofisi yake imeanza kufanyia kazi swala hilo na kwa muda wa wiki moja watatoa taarifa kamili na hatua zilizochukua ili kunusuru maisha ya watanzania wengi wanaoenda kwenye Hospitali za serikali kupatiwa huduma.

Dr.Kigwangala amesema wizara yake imepata taarifa ya baadhi ya watumishi wa Sekta hiyo kutumia Kauli ya Rais wa Awamu ya Tano Dr.John Magufuli ya Hapa kazi tu kwa kuwanyima haki ya kupata huduma wananchi pindi wanapohitaji huduma za kiafya.