Baahdi ya Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wakiwa katika moja ya Mikutano ya Chama hicho.
Baadhi ya wagombea hao waliokosa nafasi za kugombea nafasi ya kuwakilisha kwa madai hawakuwa na fedha hizo Issa Yusuph na Gabriel Adam wamesema walilazimika kutoa kati ya shilingi laki moja hadi laki tano kwa kila mjumbe ili kushawishi kupigiwa kura hatua ambayo imetajwa kusabisha kasoro kubwa katika uchaguzi huo.
Wameongeza kuwa endapo hatua za haraka hazitachukuliwa kuna hatari kubwa kwa wananchi kupoteza imani na chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Hata hivyo mwenyekiti wa CHADEMA wilaya hiyo Bw, Charles Lyanyare, amesema endapo vitendo hivyo vya rushwa vitathibika ameshauri vikao vya juu vya maamuzi kuchukua hatua kali katika kunusuru chama hicho kupasuka.
Kwa upande wake mshindi katika uchaguzi huo Bw Yusuf Kazi, ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wajumbe kwa kumchagua kwa kura 202 kati ya kura 300 zilizopigwa katika uchaguzi huo.