Serikali ya Tanzania imewahakikishia wananchi kuwa ipo tayari kukabiliana kuokoa maisha ya wananchi wake katika maafa yatakayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi likiwemo suala la usalama baharini na tetemeko la Tsunami.
Hayo yameelezwa na katibu mkuu wa wizara ya ujenzi, mawasiliano na uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mafunzo yahusuyo uelewa wa Tsunami na maandalizi ya namna ya kuzuia majanga nchini Tanzania.
Kwa upande wao mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania TMA imesema kuwa itaendelea kuwaelimisha wananchi juu ya majanga yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabia nchi huku ikieleza kuwa uelewa kwa wananchi umeongezeka kuhusu kufuatilia ushauri wa TMA kuhusu hali ya hewa hali iliyosaidi kupunguza maafa yatokanayo na tabia nchi.

