Friday , 5th Aug , 2016

Mamlaka ya mapato nchini TRA inakusudia kuanza kukusanya kodi kutoka katika gharama za upangishaji na hivi karibuni itaanza kufanya uhakiki na mahesabu ya makadirio kwa ajili ya kukusanya kodi hiyo.

Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi TRA, Bw. Richard Kayombo,

Mamlaka ya mapato nchini TRA inakusudia kuanza kukusanya kodi kutoka katika gharama za upangishaji ambapo katika kutekeleza hilo hivi karibuni itaanza kufanya uhakiki na mahesabu ya makadirio kwa lengo la kukusanya kodi kutoka kwenye majengo na nyumba za kupangisha.

Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi Bw. Richard Kayombo, amesema hayo leo na kwamba katika kutekeleza hilo amewasihi wapangaji kujiepusha na vitendo vyovyote vya udanganyifu kwa kutotoa au kuficha taarifa sahihi za mikataba na kiasi halisi cha pesa wanayolipa kama pango.

Kwa mujibu wa Kayombo, TRA kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za serikali itaanza uhakiki wa nyumba kwa nyumba kwa lengo la kubaini nyumba ambazo wakaaji wake ni wapangaji kwa lengo la kufahamu gharama wanazolipa ili kutoa makasirio sahihi ya kiasi cha kodi anachopaswa kulipa mmiliki wa nyumba husika.

Aidha Kayombo ametoa taarifa ya makusanyo ya mwezi Julai , ambapo amesema kuwa Mamlaka ya mapato nchini TRA imefanikiwa kukusanya trilioni 1.055 sawa na 95.6% ya lengo la trilioni 1.103 kwa mwezi Julai 2016.