Thursday , 14th Jul , 2016

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA imetoa mashine 130 kwa makatibu wakuu 25 wa wizara zote za Jamhuri ya mungano wa Tanzania ili kufanikisha lengo la kukusanya shilingi Trilioni 15.5 kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Kamishna mkuu wa TRA Bwana Alphayo Kidata amesema kuwa hatuo hiyo ya TRA kugawa mashine hizo nikuhakikisha kuwa taasisi zote za serikali zinatumia mashine za kiektroniki kutoa risiti kila katibu mkuu amepewa mashine za kutoa risiti tano kwaajili ya kusambaza kwenye wizara zao.

Aidha bwana Kidata, amewataka watumishi wote wa serikali ambao wanafanya marejesho ya matumizi mbalimbali kuambatanisha risiti zitolewazo na mashine za kielektroniki.

Mamlaka ya mapato TRA imesisitiza kuwakamata wanao kwepa kutumia ya mashine za Kielektroniki ikiwa pamoja na Kuwafikisha mahakamani wale wasiotumia mashine hizo ambapo bwana Kidata amewataka wananchi kulipa kodi kwa hiari.