Monday , 10th Nov , 2014

Wajasiriamali nchini wameshauriwa kuwa na macho yanayoona fursa za kibiashara na kuzitumia kujiinua kuchumi hata katika mazingira magumu.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini –TPSF Dr Reginald Mengi ametoa changamoto hiyo jijini Dar es salaam alipokutana na viongozi wa Vyama vya Wanawake Wajasiriamali Tanzania, katika mkutano ulioandaliwa kwa pamoja na Chama cha Wanawake kinachojihusisha na kazi za mikono- TAWOHATE na TPSF.

Dr Mengi amewataka wajasiriamali wayageuze matatizo wanayokabiliana nayo kuwa ni changamoto za kuwawezesha kufanikiwa kiuchumi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye amesema TPSF itaendelea kuunga mkono juhudi za Vikundi vya wanawake vya ujasiriamali kwa vile amesema utafiti waliofanya umedhihirisha kuwa wanawake wana nafasi muhimu katika kuleta maendeleo katika jamii.

Mapema mwenyekiti wa TAWOHATE Bi Anna Matinde alisema Mkutano huo ni fursa maalum kwa viongozi wa vyama vya wanawake wajasiriamali nchini kuweza kuwasiliana moja kwa moja na viongozi wakuu wa TPSF kuhusu changamoto wanazokabliana nazo.

Tags: