Tuesday , 5th Jul , 2016

Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), imesema itaendelea kuweka kipaumbele katika kutafuta fursa za uwekezaji kiuchumi na biashara kwa kuwa nchini nyingi duniani uchumi wake unakua kupitia sekta binafsi.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF,Godfrey Sembeye.

Akizungumza katika semina iliyoandaliwa na TPSF,na Shirika la Maendeleo la Japan(JICA), Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF,Godfrey Sembeye, amesema semina hiyo inawapa mwangaza watu wa sekta binafsi kujua maeneo gani yanaweza kuwapa fursa ya kupata fedha maendeleo.

Sembeye, amesema Tanzania, nchi inayopata msaada mkubwa kutoka kwa JICA, ikilinginishwa na nchi nyingine za Afrika na hivyo kusaidia sekta binafsi kufanya shughuli za maendeleo kwa kutengeneza miundombinu ili kuweza kufanya biashara.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkuu wa JICA,Toshia Nagase, amesema mkutano huo umelenga kuibua fursa zilizopo katika uwekezaji wa sekta binafsi na hatimaye kukuza maendeleo ya kiuchumi nchini.