
Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya la Taifa la Biashara nchini.
Mwenyekiti wa kamati ya utendaji ya baraza hilo, Balozi John Kijazi amesema hayo alipokutana na wajumbe wa kamati ya baraza hilo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Balozi Kijazi ambaye pia ni katibu Mkuu Kiongozi amesema kuwa wamejipanga kutekeleza nia ya kufikia uchumi wa kati kupitia sera ya Viwada nchini Tanzania.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa TNBC, Mhandisi Raymond Mbilinyi amesema kwa sasa baraza lina jukumu la kuhakikisha uwekezaji katika viwanda unakua na kwamba ni jambo la umuhimu kwa sekta za umma na binafsi kushirikiana na kutekeleza jambo hilo.
Mbilinyi amesema licha ya kuwapo jitihada hizo za kukuza uwekezaji wa viwanda pia wanalenga kuimarisha mabaraza ya mikoa na wilaya ili yafanye kazi zake kwa ufanisi.