Tuesday , 1st Sep , 2015

Wanawake nchini Tanzania kupitia mtandao wa Jinsia TGNP wameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi isimamie vyema Uchaguzi ili uwe wa Haki, Huru na kujali Usawa wa kijinsia.

Makamu Mkurugenzi wa Tamwa Eda sanga akisisitiza jambo kwenye mkutano

Tamko hilo kwa Niaba ya wanawake wote nchini limetolewa leo jijin Dar es salaam na Makamu Mkurugenzi wa TAMWA Eda Sanga katika Tamasha la jinsia lililoandaliwa na TGNP mtandao na kushirikisha vikundi 65 vya wanawake, vyama vya siasa na wadau mbalimbali wa Maendeleo.

Bi Eda sana amesema chama kitakachoshinda uchaguzi ni lazima kihakikishe wanawake wanapata afya njema, Maji, Elimu, Hifadhi ya Jamii pamoja na kuwalinda wanawake, walemavu, watoto, wazee na makundi maalumu.

Aidha Eda Sanga amewataka wanawake wasiuze kura zao kwa wagombea na kuitaka TAKUKURU kuhakikisha inadhibiti Rushwa katika Uchaguzi kwani Rushwa imekithiri, wakati huohuo wanawake nchini wamesema kuwa wanawake ndiyo wazalishaji wakubwa na lazima mchango wao uthaminiwe.