Tuesday , 26th Apr , 2016

Serikali Mkoani Mtwara imewataka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kupunguza tozo katika mbao zinazosafirishwa kwenda sehemu mbalimbali mkoani humo kwa ajili ya kutengezea madawati kwa matumizi ya wananfunzi wa shule za msingi na sekondari.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally,

Akizungumza baada ya kutembelea karakana ya kutengenezea madawati ya halmashauri ya wilaya, iliyopo katika manispaa ya Mtwara Mikindani, Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, amesema jitihada mbalimbali zinafanyika kwa ajili ya kutafuta fedha za kutatua tatizo hilo lakini fedha nyingi zinatumika katika kilipia tozo hizo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara, Zacharia Nachoa, amezitaka jamii kuunga mkono jitihada hizo zinazofanywa na viongozi wao za kutatua changamoto hiyo huku akiwapongeza wananchi wa tarafa ya Ziwani ambao kupitia kata zao wamehamasika kwa kiasi kikubwa kuchangia kwa hiyari utatuzi wa tatizo hilo.

Salumu Juma, mkazi wa manispaa ya Mtwara, ameipongeza serikali ya wilaya na mkoa kwa ujumla kwa jitihada za dhati wanazozifanya katika kuhakikisha wanawaokoa wanafunzi kutoka katika adha ya kukaa chini..

Sauti Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally,akizungumza TFS kupunguza tozo la Mbao za madawati