Friday , 6th May , 2016

Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imejipanga kudhibiti uingizwaji wa bidhaa bandia na duni katika mipaka ya nchi ikiwemo mpaka wa Namanga kwa kuongeza doria katika mpaka huo kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali.

Mkurugenzi wa TFDA nchini Hiiti Siilo, Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa TFDA Bw. Raymond Wigenge, na Meneja wa Ukaguzi wa Chakula wa TFDA kanda ya Mashariki Bw. Emmanuel Alphonce.

Akizungumza katika ziara ya Maafisa wa TFDA waliotembelea Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Nchi za Afrika Mashariki, Mkurugenzi Uenezaji wa Huduma katika mamlaka hiyo amesema kuwa kituo hicho kitaongeza ufanisi katika udhibiti wa bidhaa bandia.

Mwanasheria wa TFDA, Eskari Fute, amesema kuwa kumekuwepo na changamoto ya udhibiti ili bidhaa iliyokatazwa kwenye nchi moja isiruhusiwe katika nchi nyingine ili kuondoa mianya itakayosababishwa na sheria hivyo kupendekeza vigezo vya kuruhusu bidhaa vifanane.

Afisa Forodha wa TRA, Aminieli Lewis, amesema kuwa licha ya kufanya kazi ya kukusanya mapato pia wamekua wakishirikiana katika kudhibiti bidhaa bandia pale wanapotilia mashaka bidhaa hizo.

Kituo cha Pamoja cha Forodha kitasaidia kuongeza ufanisi wa biashara na kupunguza urasimu katika biashara kwenye nchi mwanachama wa Afrika Mashariki.