Naibu Waziri wa Nishati na madini nchini Tanzania, Steven Masele.
Akiongea leo jijini Dar es salaam, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Steven Maselle wakati akizungumza na wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi juu ya uelewa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu nishati ya umeme.
Mhe. Maselle amesema viongozi hao washirikiane kwa pamoja na wizara yake ili kutatua migogoro ya wachimbaji wadogo kwa kuwaelimisha wananchi juu ya sheria na taratibu za sekta ya nishati na madini ikiwa ni pamoja na taratibu za uchimbaji madini.