Thursday , 24th Jul , 2014

Wananchi mkoani Lindi wanatarajia kuelimishwa njia bora na za kisasa za uvuvi, ufugaji na ukulima ili waweze kuongeza kipato chao na taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG Group Imani Kajula (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakulima Tanzania(TASO) Bw. Engelbert Moyo, amesema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akiongelea kuhusu maonesho ya kilimo Nane Nane ambayo Kitaifa yatafanyika mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa Moyo, wananchi watajifunza teknolojia mpya za kilimo, ufugaji na uvuvi ili waweze kuzalisha mazao yanayokidhi viwango vya Kitaifa na Kimataifa huku wavuvi wakipewa elimu juu ya madhara ya uvuvi haramu na unavyohatarisha mazingira na viumbe wa majini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni ya EAG Group ambayo ni washirika wa maonesho hayo Bw. Imani Kajula amesema uimarishwaji wa Miundo mbinu katika sekta ya kilimo ni moja ya njia za kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira nchini Tanzania pamoja na mataifa mengine machanga yanayoendelea Duiniani.

Katika hatua nyingine, viwanda vya utengenezaji wa bia na pombe kali nchini Tanzania vipo hatarini kufungwa endapo serikali haitapunguza ongezeko la kodi la asilimia 20 kinyume na tozo la asilimia 10 iliyopitishwa na Bunge.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mwakilishi wa wenye viwanda hivyo, David Mgwasa, amesema uamuzi wa kupandisha kodi kumewafanya washindwe kulipa kodi na iwapo serikali haitapunguza kodi hiyo baadhi ya viwanda vitafugngwa ili kumudu ongezeko la kodi hiyo.

Ameongeza kuwa viwanda vya bia na vinywaji vikali vinapambana na ushindani kutoka bidhaa za nje zinazoingia nchini kinyume cha sheria jambo linaloweza kuufanya uchumi ukshuka iwapo hali hiyo haitadhibitiwa.