
Hayo yamethibitishwa na Waziri wa Afya Dkt, Ummy Mwalimu ambaye amesema kwamba upasuaji huo nib juhudi za serikali kuokoa fedha ambazo zingelipwa nje ya nchi kugharamia matibabu hayo na badala yake fedha hizo zitumike kuleta maendeleo kwenye maeneo mengine yenye uhitaji nchini.
Aidha Waziri Ummy amesema kwamba kwa zaidi ya mwaka Hospitali ya Taifa ilijikita kuwekeza kwenye kuongeza ujuzi wa wataalamu wa aina mbalimbali wakiwemo wa upasuaji wa kupandikiza figo na kwamba wataalamu 19 walipelekwa nchini India, na Norway kwa ajili ya utaalam,u wa mafunzo hayo.
"Kuanzishwa kwa huduma hapa nchini kutaleta unafuu katika gharama na hivyo kutasababisha wagonjwa wengi zaidi kutibiwa . Takribani wagonjwa 400 wanakadiriwa kuwa katika huduma hii katika vituo mbalimbali hapa nchini ambapo kwa hospitali ya Muhimbili wanaopata huduma kwa sasa wapo 200 na waliobakia ni wapo katika vituo mbalimbali vya Serikali na Binafsi" Ummy.
Aidha imeelezwa kwamba utayarishaji wa mgonjwa kwa ajili ya matibabu ya upandikizaji figo ikiwemo vipimo mbalimbali vinavyohitajika kwa mpokeaji figo na mtoaji unagharimu takribani milioni 21 kiasi ambacho ni cha chini tofauti na hapo awali ambapo serikali ilikuwa ikigharamia milion 80-100 kwa mgonjwa mmoja huku ikidaiwa kwa mwaka walikuwa wanasafirishwa wagonjwa hadi 35