Wednesday , 6th Apr , 2016

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imeanza kutekeleza mpango wa Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la maendeleo ya viwanda UNIDO.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imeanza kutekeleza mpango wa Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la maendeleo ya viwanda la Umoja wa Mataifa UNIDO kutangaza kuwepo kwa muongo wa viwanda barani Afrika.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam katika mkutano wa 21 uliowakutanisha wasomi na watafiti, wanaotafiti masuala ya maendeleo na uchumi duniani kutoka nchi mbali mbali kwa lengo la kutekeleza mpango wa pili wa serikali wa miaka mitano unaoanza mwaka ujao wa fedha 2016 mpaka mwaka 2021 unaojielekeza kwenye uchumi wa viwanda kwa kutumia rasilimali zilizopo nchini.

Mhe. Suluhu amesema taifa linashirikiana na nchi wahisani duniani katika kuhakikisha wanabadilishana uzoefu na nchi nyingine hasa zile zilizoendelea zaidi duniani.

Kwa upande wake mdau wa maendeleo na Mchumi Mwandamizi nchini Prof. Samweli wangwe amessisitiza kwa Tanzania itumie watafiti wake wa ndani kufanya tafiti katika kuongeza maendeleo ya nchi na umuhimu wakuimarisha nguvu kazi za watanzania hasa waliopo vyuoni katika kuwajengea uwezo wa ziada wakubuni njia zakuleta maendeleo ya nchi.