
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Selimundu (Sickle Cell) duniani na mtaalam wa ugonjwa huo, Dkt. Deogratius Soka ambapo amesema asilimia 70 ya watoto wanaozaliwa na tatizo hilo duniani hufariki dunia wakiwa chini ya umri wa miaka miwili.
Dkt. Soka amesema nivyema serikali ikaweka mikakati mbalimbali ya kuwalinda watoto kabla hawajapata madhara yatokanayo na ugonjwa huo kuliko ilivyo hivi sasa ambapo watu wengi hubaini ugonjwa huo ukiwa umeshaleta adhari mbalimbali.
Dkt. Soka ameshauri jamii hasa vijana kupima afya zao na wenza wao kabla ya kuamua kupata watoto ili kuweza kuepuka kupata watoto wenye ugonjwa huo au kuwalinda watoto wao mapema ili kupunguza madhara yatokanayo na ugonjwa huo.
Akitaja dalili za ugonjwa huo Dr. Soka amesema nipamoja na maumivu makali ya viungo, kuvimba kwa maungio kama vile vidole au miguu na sehemu zingine zinazo unganisha mwili, kupungukiwa damu mara kwa mara, homa za mara kwa mara, homa ya manjano pamoja na matatizo mengine ikiwemo matatizo ya ini.
Dr Soka pia amesema ili kujilinda na madhara ya mara kwa mara ni vyema mgonjwa wa Sikle Cell apewe maji mengi kwa kiwango cha lita 3 hadi 4 kwa siku, kukaa sehemu yenye hewa safi, kuepuka shuguli zinazo chosha mwili na uchovu kupitiliza.
Hata hivyo waalimu mashuleni wametakiwa kuacha kutoa adhabu kali kwa watoto wenye Sikle Cell ili kuwalinda dhidi ya madhara ya kiafya wanayoweza kupata kutokana na adhabu wanatoa kwa watoto wenye sikle cell.