
Waziri wa afya na ustawi wa jamii nchini Tanzania, Dkt Seif Rashid.
Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Mganga Mkuu wa serikali Dk. Donald Mmbando wakati wa maadhimisho ya siku ya wakunga na wauguzi yaliyoanza kuadhimishwa katika hospital ya taifa ya Muhimbili huku maadhimisho hayo yakiwa na ujumbe usemao Dunia inahitaji Wakunga wenye Ujuzi sasa Kuliko wakati Mwingine.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Rais wa Chama cha Wakunga nchini Tanzania Feddy Mwanga amesema uhaba wa vifaa na wingi wa wakina Mama wanaokwenda kujifungua ni moja ya sababu inayochangia vifo vya watoto