
Hali hiyo inatokana na takwimu kuonyesha kuwa kwa sasa daktari mmoja anawahudumia wagonjwa wapatao milioni mbili kwa mwaka hatua inayopunguza ufanisi katika utoaji tiba ya usingizi.
Hayo yameelezwa Jijini Dar es Salaam na Wataalam wa kutoa Dawa za Maumivu na Usingizi kutoka nchi mbalimbali duniani zikiwemo zile za Afrika Mashariki, katika mkutano ulioandaliwa na chama cha Madaktari Bingwa wa kutoa Dawa za Usingizi na Maumivu (SATA) uliokuwa unajadili mambo mbalimbali yahusuyo
fani hiyo pamoja na changamoto zake.
Akizungumza katika mkutano huo, Rais wa chama cha SATA Dk. Mpoki Ulisubyisye amesema changamoto kubwa ni ujuzi wa kutumia vifaa vilivyopo hivyo madaktari wanapaswa kutambua dawa salama kwa mgonjwa ambazo zitaweza kumsaidia wakati anapoumwa.