Mwenyekiti wa chama cha MVIWATA Elizabeth Masanja.
Tahadhari hiyo imetolewa na wakulima mkoani Kilimanjaro katika warsha ya kujadili changamoto zinazomkabili mkulima mdogo iliyoandaliwa na mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania(MVIWATA)
Wakulima hao wamedai kuwa serikali ikitumia fedha nyingi katika warsha na semina ambazo zimekuwa hazimfikii mkulima mdogo na kujua changamoto zinazomkabili hivyo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Wamesema nchi ipo kwenye hali ya hatari ya kukumbwa na njaa kutokana na na wakulima kushindwa kuendesha kilimo cha kisasa na chenye tija kutokana na kuwa na mitaji midogo ya kununulia pembejeo kukosa ellimu ya kilimo cha kisasa na kudidimiza sekta ya kilimo.
Naye mkulima Martha Boma kutoka wilaya ya Monduli amesema bado kilimo ni changamoto nchini kutokana na sera ya kilimo kukosa nguvu ya kuibana serikali kuwasimamia na kuwashirkisha wakulima wadogo kutoa maamuzi ya kuhsu kilimo.
Kwa upande wake mtaalamu wa kilimo kutoka MVIWATA Godfrey Kabuka amesema kuna haja kwa serikali kuangalia uwezekano wa kutoa mrejesho kwa wakulima wadogo ili kuinua kipato chao.